You are currently viewing Tanzania ilivyoandika historia kupunguza vifo vya uzazi

Tanzania ilivyoandika historia kupunguza vifo vya uzazi

Rais Samia Suluhu Hassan amesema vifo vya uzazi Tanzania vimepungua hadi 76 mwaka 2024/25 kutoka 104 vilivyorekodiwa awali, hatua inayokaribia kufikia lengo la maendeleo endelevu (SDG) la vifo 70 kwa vizazi hai 100,000.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Novemba 26, 2026 katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa tatu wa kisayansi wa afya jijini Dar es Salaam.

Amesema anaamini Tanzania itafikia lengo hilo la SDG ifikapo mwaka 2030, akisisitiza kuwa nchi inakosa vifo sita tu kufikia kiwango kinachotakiwa kimataifa.

Kwa upande wa vifo vya watoto wachanga, amesema vimepungua kutoka 24 hadi 17 kwa kila vizazi hai 1,000, huku lengo la dunia likiwa 15.

Rais Samia amesema katika vya watoto chini ya miaka mitano navyo vimepungua kutoka 43 hadi 28 kwa kila vizazi hai 1,000, wakati lengo la maendeleo endelevu ni 25.

Amesema mafanikio hayo yanaonyesha kuwa inawezekana kupunguza vifo kwa kuweka nia na kusimamia juhudi, akieleza matumaini ya Tanzania kufikia malengo hayo ifikapo 2030.