Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeunda timu ya wataalamu wa uchunguzi wa ajali ili kubaini chanzo cha tukio la meli ya MV Mwanza kugonga mwamba wa Bismarck (Bismarck Rock) katika Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TASAC leo, Novemba 18, 2026, tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:29 asubuhi wakati meli hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) ikiwa safarini kutoka Bandari ya Mwanza Kusini kuelekea Mwanza Kaskazini.
TASAC imeeleza kuwa baada ya tukio hilo, meli ilirejea salama katika Bandari ya Mwanza Kusini majira ya saa 6:12 mchana, huku abiria na wafanyakazi wote waliokuwa ndani ya meli wakishuka salama.
Shirika hilo limethibitisha kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa, na hakuna uchafuzi wa mazingira uliotokea.
TASAC imeongeza kuwa matokeo ya awali ya uchunguzi huo yatatolewa kwa umma mara baada ya kukamilika kwa kazi ya timu ya wataalamu.
Endelea kufuatilia Mchukuzi TV kwa taarifa zaidi kuhusu usafiri, uchukuzi na maendeleo ya sekta ya usafirishaji nchini.
