Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2024, ambapo watahiniwa 477,262 kati ya wanafunzi 516,695 wenye matokeo wamefaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III na IV.
NECTA imesema ufaulu huo umepanda kwa asilimia 3, hivyo kufikia asilimia 92.37 kutoka asilimia 89.36 mwaka 2023.
Aidha, kwa mwaka 2024, takwimu zinaonesha idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya I, II na III imeongezeka na kufikia 221,953 sawa na asilimia 43, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo idadi ilikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.4.
Akitangaza matokeo hayo leo tarehe 23 Januari mwaka huu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dk. Said Mohamed amesema idadi ya watahiniwa waliopata daraja la IV na 0 imepungua, hivyo ubora wa ufaulu umepanda kwa asilimia 5.6.
Mohammed amesema ubora wa ufaulu wa madaraja ya ni mzuri zaidi kwa wavulana ikilinganishwa na wasichana ambapo wavulana ni 119,869 sawa na asilimia 48.90 ya wavulana wote wenye matokeo na wasichana ni 102,084 sawa na asilimia 37.59 ya wasichana wote wenye matokeo.
Bofya hapa kutazama matokeo hayo;
https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/csee/CSEE2024/CSEE2024.htm