Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Ujenzi na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na Bodi ya Usajili wa Wakadiriaji Majenzi na Wabunifu Majengo (AQRB) na Taasisi mbalimbali wakiwa katika kikao kazi cha mapitio ya taarifa ya utafiti wa maboresho ya utendaji wa bodi za ERB, CRB na AQRB Mkoani Morogoro leo tarehe 03 Juni 2025.
