You are currently viewing Marekani yaidhinisha dawa inayokinga VVU kwa 99.9%

Marekani yaidhinisha dawa inayokinga VVU kwa 99.9%

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani imeidhinisha sindano ya kampuni ya Gilead Sciences- Lenacapavir, kudungwa mara mbili kwa mwaka katika kuzuia Virusi Vya Ukimwi (VVU) vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI katika mwili wa binaadamu, hatua ambayo inatazamwa kama mafanikio makubwa katika vita dhidi ya virusi vya ugonjwa wa huo.

Dawa za kuzuia maambukizi ya VVU, zinazojulikana kama pre-exposure prophylaxis au PrEP, zimekuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Kwa kawaida huhitaji kumeza kidonge kila siku, na bado haziwajaweza kufanya uharibifu mkubwa kwa walioambukizi virusi hivyo kote ulimwenguni.

Mwenyekiti wa Gileadi na mtendaji mkuu Daniel O’Day amenukuliwa katika taarifa akisema “Hii ni siku ya kihistoria katika mapambano ya miongo kadhaa dhidi ya VVU.”

Lenacapavir, ambayo ipo sokoni kwa jina la chapa Yeztugo, imeonyesha kupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa zaidi ya asilimia 99.9 kwa watu wazima na vijana na kuifanya kiutendaji kuwa sawa na chanjo yenye nguvu. Je hatua hii itakuwa na matokeo gani kwa umma?

Leave a Reply