You are currently viewing Wenje ataja sababu kuhamia CCM

Wenje ataja sababu kuhamia CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Victoria, Ezekiah Wenje ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uamuzi wa Wenje, unakuja katikati ya nyakati ambazo, Chadema imepoteza maelfu ya wanachama wake, waliojiunga na vyama mbalimbali vya siasa, baada ya chama hicho kutangaza kususia Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wenje ametangaza kujiunga na CCM leo, Jumatatu Oktoba 13, 2025 katika mkutano wa kampeni za urais za Dkt Samia Suluhu Hassan, zilizofanyika Chato mkoani Geita.

Kwa mujibu wa Wenje, uamuzi wake wa kuhamia CCM umetokana na kiu yake ya kutumia maarifa aliyonayo kushauri kwa mustakabali mzuri wa Taifa, huku akidokeza chama hicho kimefanya kazi kubwa hasa ya kulinda amani tangu uhuru.

Sambamba na hilo, Wenje aliyewahi kuwa Mbunge wa Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, amesema chama chake cha zamani kinapaswa kupuuzwa kuhusu madai ya kuzuiwa na Serikali kushirikli uchaguzi, kwa kuwa kilifanya uamuzi huo chenyewe.

Leave a Reply