You are currently viewing WHO yatoa bil. 7 kukabili Marburg, mmoja abainika kuambukizwa

WHO yatoa bil. 7 kukabili Marburg, mmoja abainika kuambukizwa

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limeipatia Tanzania shilingi bilioni 7.56, ili kudhiti na kukabiliana na ugonjwa wa Marburg nchini.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameyasema hayo, leo Jumatatu Ikulu ya Chamwino, Dodoma, akizungumza na kwenye mkutano na Rais Samia Suluhu Hassan.

Awali, akizungumza katika mkutano huo, Rais Samia amesema kwamba serikali ilichukua hatua kufuatia uvumi uliokuwa ukiendelea katika eneo la Kagera.

Amesema kwamba sampuli zilizochukuliwa katika hospitali moja mjini Kagera na kuthibitishwa mjini Dar es Salaam zilimtambua mtu mmoja aliyekuwa na virusi vya maradhi hayo .

Hata hivyo, sampuli za washukiwa wengine wa maradhi hayo hazikupatikana na ugonjwa huo hatari.

Rais Samia amesema kuwa hii ni mara ya pili kwa virusi vya maradhi hayo kugunduliwa nchini Tanzania mara ya kwanza vikigunduliwa mnamo mwezi Machi 2023 katika eneo hilohilo la Kagera wilayani Bukoba.

Ameongezea kwamba kufikia sasa kumekuwepo na visa 25 vya washukiwa wa maradhi hayo ambapo sampuli zao zimepatikana hazina ugonjwa huo na kwamba serikali inawafuatilia kwa karibu.

Amesema kwamba uvumi uliokuwa ukiendelea katika eneo hilo kwamba kuna baadhi ya watu waliofariki haujathibitishwa na kwamba serikali yake inafanya kila juhudi kubaini chanzo cha vifo hivyo.

Alilishukuru shirika la WHO kwa kuchukua hatua za dharura akisema kwamba serikali yake itachukua hatua kama zile zilizochukuliwa mwaka 2023 kudhibiti maradhi hayo.

Kwa upande wake katibu mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus mbali na ufadhili ametoa ufadhili wa dola za Marekani milioni tatu, amesema kufikia sasa hakuna chanjo wala tiba iliothibitishwa kukabiliana na virusi vya Marburg licha ya kwamba kuna mipango ya kuafikia hayo.

Hatahivyo aliongezea kuwa milipuko inaweza kudhibitiwa kupitia mikakati ya kuzuia maambukizi na kuokoa maisha kama ilivyofanya Tanzania.

Leave a Reply