You are currently viewing Hakuna kuvua viatu kwenye ukaguzi viwanja vya Marekani

Hakuna kuvua viatu kwenye ukaguzi viwanja vya Marekani

Viwanja vya ndege vya Marekani havitahitaji tena abiria kuvua viatu vyao wakati wa ukaguzi wa usalama unaoendeshwa na Utawala wa Usalama wa Usafiri (TSA) – ukiondoa sera hiyo isiyopendwa na watu baada ya miongo miwili.

Katibu wa Usalama wa Ndani, Kristi Noem alisema mabadiliko hayo yalianza kutumika mara moja kwa viwanja vya ndege kote Marekani, ingawa mchakato wa ukaguzi wa usalama wa viwango kadhaa utasalia.

Aidha, Noem amesema abiria lazima bado wataendelea mikanda na makoti na watoe tarakilishi zao na vinywaji kutoka kwenye mikoba, lakini sheria hizo pia zinapitiwa upya.

Sharti la abiria wa ndege kuvua viatu ili kufanyiwa ukaguzi lilianza kutekelezwa nchi nzima tangu 2006 baada ya Muingereza kuficha bomu katika kiatu chake kimoja akiwa kwenye safari ya ndege ya kuelekea Miami.

Noem aliwaambia waandishi wa Habari jana Jumanne kuwa; “Teknolojia yetu ya usalama imebadilika sana. TSA imebadilika.

“Tuna mfumo mpana, unaojumuisha serikali nzima katika suala la usalama na mazingira ambayo watu wanatazamia na kupitia wanapoingia kwenye uwanja wa ndege ambao umeboreshwa.”

Katibu wa usalama wa ndani aliongeza: “Ni muhimu kutafuta njia za kuwaweka watu salama, lakini pia kurekebisha na kufanya mchakato huo kuwa wa kufurahisha zaidi kwa kila mtu.”

Leave a Reply