Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile, amesema idadi ya wataalamu katika sekta ya anga nchini imefikia jumla ya wataalamu 3,993 hadi kufikia Januari 2026.
Kihenzile aliyasema hayo aliposhiriki katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania @officialtcaa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi hiyo inajumuisha marubani 566, wahandisi wa ndege 118, waongozaji wa ndege 144, wahudumu wa ndege 583, maafisa wa uendeshaji wa safari za ndege 312, wataalamu wa usalama wa viwanja vya ndege 2,080, marubani wa ndege zisizo na rubani 66 pamoja na wanafunzi wa urubani 80.
Aidha, amesema sekta ya anga imeendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa mapato ya Serikali kupitia ushuru pamoja na tozo mbalimbali za usafiri wa anga zinazolipwa na mashirika mbalimbali katika sekta ya anga.
Vilevile, ameongeza kuwa Tanzania imeingia katika mikataba ya kudumu ya usafiri wa anga na nchi 21, hatua iliyosaidia kuvutia mashirika mengi ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari mpya za ndege nchini.
Katika kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 2025 hadi Desemba 2025, sekta ya anga ilionyesha ukuaji mkubwa, hususan kuongezeka kwa idadi ya miruko ya ndege, ambapo idadi ya miruko ilifikia 189,505 ikijumuisha safari za ndani na za kimataifa. Wakati huo huo, abiria waliopanda ndege walifikia 4,456,215 na mizigo iliyosafirishwa ilifikia zaidi ya tano 20,400.
