You are currently viewing JWTZ wapokea ndege ya kijeshi kutoka Falme za Kiarabu (UAE)

JWTZ wapokea ndege ya kijeshi kutoka Falme za Kiarabu (UAE)

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Lawrence Tax leo amepokea ndege ya kijeshi kutoka Jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Falme za Kiarabu.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo Dk. Tax ameshukuru na kusema ushirikiano huo uendelee kwa manufaa ya pande zote mbili.

Amesema ndege hiyo itatumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo, kusafirisha viongozi mbalimbali wa kiraia na kiserikali, usafirishaji wa kijeshi na kudondosha askari wa miavuli.

“Mashirikiano haya yanayoendelea kati ya jeshi letu na jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu, serikali anayoiongoza rais wetu, Samia ni kudumisha mahusiano mazuri na nchi rafiki. Jeshi letu lipo tayari kutekeleza majukumu yetu ndani na nje ya nchi na kuhakikisha inakuwa salama,” alisema Waziri Tax.

Leave a Reply