You are currently viewing Ziara ya Dkt Samia Urusi kuimarisha taswira, hadhi ya Tanzania kimataifa

Ziara ya Dkt Samia Urusi kuimarisha taswira, hadhi ya Tanzania kimataifa

Mchambuzi wa masuala ya Diplomasia, Leonard Chakupewa, amesema ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nchini Urusi, inaipa Tanzania nafasi ya kuimarisha taswira na hadhi yake kimataifa na fursa ya kueleza kwa upana mageuzi, hatua na mipango yake.

Dkt Samia, anakuwa mkuu wa nchi wa pili wa Tanzania kufanya ziara nchini Urusi, baada ya miaka 57 tangu Rais wa kwanza hayati Mwalimu Julius Nyerere, afanye ziara katika Taifa hilo mwaka 1969.

Katika ziara hiyo, Dkt Samia ameingia Ikulu ya Urusi ya Kremel na kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi na mwenyeji wake, Rais wa Taifa hilo, Vradmir Putin.

Akichambua fursa za ziara hiyo katika kipindi maalumu kilichorushwa na Shirika la Utangazahi Tanzania (TBC), Chakupewa amesema ziara hiyo ni fursa ya Tanzania kuielezea dunia mwelekeo wake, hasa kuifafanua Dira yake ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Hatua hiyo, amesema itaifanya Tanzania kuvutia uwekezaji wa maeneo mbalimbali kutoka Urusi, kukuza biashara na uchumi wake, hasa ukizingatia kuna mikataba mbalimbali inayosainiwa.