You are currently viewing Rais Samia: Kodi ndizo tunazotumia kuhudumia wananchi

Rais Samia: Kodi ndizo tunazotumia kuhudumia wananchi

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kodi zinazokusanywa na mapato mengine, ndizo zitakazoiwezesha Serikali kuendelea kuendesha baadhi ya huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo leo, Jumatano Julai 1, 2026 alipozungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na utoaji wa Tuzo za Rais kwa Walipakodi.

“Nathubutu kusema kuwa, kulipa kodi ni wajibu wa kila mmoja wetu katika kujenga Taifa linalojitegemea. Kulipakodi ni uzalendo na ushujaa kwa maendeleo na kujitegemea kwa Taifa letu,” amesema.

Amesema uzalendo huo lazima uwe wa pande zote, mwekezaji alipe kodi kwa uaminifu, mamlaka ya mapato ikusanye kwa haki na Serikali itumie kwa uadilifu.