You are currently viewing KIZIMKAZI KUMENOGA, SHANGWE NA FURSA

KIZIMKAZI KUMENOGA, SHANGWE NA FURSA

Kizimkazi inakuita! Kuanzia Agosti 12–14, 2026, jiandae kwa siku tatu za utalii, biashara, burudani na fursa za uchumi wa buluu katika mandhari ya kuvutia.

Shangwe inaanzia Agosti 12 kwa matembezi ya pamoja yakifuatiwa na maonyesho ya biashara, kisha tunakutana kwenye mdahalo wa uchumi wa buluu na mashindano ya ngalawa katika mwambao wa Bahari ya Hindi na fursa za kukutana na kujenga ushirikiano.

Agosti 13, shuhudia uzinduzi wa miradi ya maendeleo, kisha usiku uwashe kwa burudani ya Kizimkazi Night itakayokusanya wasanii, wageni kutoka nje ya Tanzania na maelfu ya wananchi.

Agosti 14, tamasha linafikia kilele chake kwa kusherehekea urithi wa Kizimkazi, vivutio vya utalii na fursa zinazofungua milango ya maendeleo. Karibu Kizimkazi Festival mahali ambapo shangwe inakutana na fursa.