You are currently viewing Samia, Tshisekedi wafungua ukurasa mpya sekta ya madini

Samia, Tshisekedi wafungua ukurasa mpya sekta ya madini

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Jamhuri ya Demokrasua ya Kongo (DRC), wamekubaliana kushirikiana kwenye sekta ya madini katika kubadilisha uzoefu na ujuzi, uchimbaji madini na uongezaji thamani na masoko.

Aidha, Rais Samia ameialika DRC, kuungana na Tanzania katika Kituo cha Madini kwaajili ya nchi za Afrika Mashariki na Kati katika kubadilishana ujuzi na tafiti.

Rais Samia na Rais wa DRC, Felix Tshisekedi wameingia makubaliano hayo leo Agosti 18, 2026, Ikulu Ndogo Zanzibar na kuzungumza na waandishi wa habari katika ziara yake ya siku mbili nchini.

Naye Rais Tshisekedi, amesema wamekubaliana na Rais Samia kubadilisha rasilimali ndani ya bara la Afrika ikiwamo sekta ya madini.

Amesema wanatakiwa kuona namna gani wanaweza kubadili sekta hiyo kwasababu wamechoka kuona rasilimali zna madini zinibiwa na inawezekana kutimiza lengo hilo kwasababu kuna rasilimali za kutosha.

Amesema pia ili kufanikisha hilo kunatakiwa kuwa na miundombinu ya kutosha, bandari, barabara, umeme na kutengeneza nishati ya kiwango cha juu zaidi ili kufanikisha hilo.

Ameahidi kuwa wapo tayari kusimama ili kuhakikisha wanatimiza malengo hayo na kuhakikisha wananchi wa Bara la Afrika wananufaika.

Amesema ushirikiano huo nan chi nyingine za afrika unafuatiliwa na mataifa mengine yakiwamo ya Bara la Ulaya na wanafahamu kuhusu maono hayo.