India imesema inataka kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika teknolojia, ubunifu na akili bandia (AI), ikieleza kuwa utaalamu wa kiteknolojia wa India unaweza kuunganishwa na rasilimali na fursa zilizopo Tanzania.
Akizungumza katika mahojiano maalum kando ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Arusha, Mbunge na Mwakilishi wa India katika Mkutano huo, Dkt. Sasmit Patra, amesema Tanzania ina mazingira na uwezo mkubwa wa kushirikiana na India katika teknolojia na kuharakisha maendeleo.
“India ina uwezo mkubwa wa teknolojia, wakati Tanzania ina rasilimali nyingi. Vyote hivi vikijumuishwa vinaweza kuimarisha Global South, na India inaiona Tanzania kama mshirika, rafiki na mwenzake barani Afrika,” amesema.
#IPU153Tanzania
