Rais Samia Suluhu Hassan, ametaka kutambuliwa na kuzawadiwa kwa wilaya na halmashauri zilizofanya vizuri katika kupunguza vifo vya uzazi.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Novemba 26, 2026 alipohutubia mkutano wa tatu wa kisayansi wa afya jijini Dar es Salaam.
Amezitaja Wilaya za Chalinze na Songwe ambazo ndani ya miezi mitatu hospitali zake hazikuwa na kifo cha mama wala mtoto kutokana na uzazi.
Ameeleza hatua hiyo itakuwa chachu kwa wauguzi na wakunga kuwa na umakini katika ulinzi wa afya ya mama na mtoto wakati wa uzazi.
