You are currently viewing Dk. Biteko awaongoza wananchi Bulangwa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa

Dk. Biteko awaongoza wananchi Bulangwa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo tarehe 27 Novemba 2024 amewaongoza wananchi wa Kata ya Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita kupiga kura kuwachagua viongozi wa ngazi ya Serikali za Mitaa.

Dk. Biteko ametimiza haki yake ya Kikatiba na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Dkt. Biteko amesema hayo baada ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita.

“Zoezi la kupiga kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi nawapongeza kwa hilo. Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti kwa sababu ya hamasa kubwa ya kushiriki,” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “ Ninaomba watu wote waliojiandikisha watumie haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kwa wingi na kwenda kupiga kura,”

Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizinduliwa Novemba 20, 2024 na kuhitimishwa Novemba 26, 2024 baada ya wagonbea kujinadi na kuomba kura kwa wananchi.

Leave a Reply