You are currently viewing Dkt. Samia: Tutajiepusha na athari za kupanda bei ya mafuta

Dkt. Samia: Tutajiepusha na athari za kupanda bei ya mafuta

Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema mradi wa ujenzi wa matenki ya kupokea mafuta, utaimarisha na kutoa hakikisho la usalama wa nishati ya mafuta kwa Taifa.

Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo leo, Jumanne Machi 3, 2026 wakati wa hotuba yake katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa matenki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema mradi huo utaimarisha akiba ya mafuta ya kimkakati ya Taifa na kuiongezea nchi uwezo wa kujilinda dhidi ya misukosuko ya kimataifa inayosababisha mabadiliko ya bei ya nishati hiyo.

“Misukosuko iliyotokea wiki iliyopita na tunayoendelea nayo tayari imeshapandisha bei ya mafuta kwa asilimia 13 mpaka jana. Sasa hatujui leo na siku zinazokwenda, lakini tumuombe Mungu watu wale wakae juu ya meza wazungumze wakubaliane ili misukosuko iishe,” amesema.

Leave a Reply