You are currently viewing Magari ya anga yaanza kuwa ukweli! je, Tanzania ipo tayari?

Magari ya anga yaanza kuwa ukweli! je, Tanzania ipo tayari?

Dunia inaingia katika enzi mpya ya usafiri baada ya jimbo la Florida nchini Marekani kufanya majaribio ya ndege mbili zinazotumia umeme, maarufu kama Flying Cars.

Ndege hizo aina ya eVTOL zilipaa na kutua wima, zikisafiri kutoka St. Petersburg hadi Tampa International Airport, katika safari iliyofuata njia ya kihistoria iliyotumiwa na ndege ya kwanza ya kibiashara mwaka 1914.

Gavana wa Florida, Ron DeSantis, alitangaza rasmi kuanza kwa mfululizo wa safari hizo za majaribio zinazoongozwa na Idara ya Uchukuzi ya Florida (FDOT), kupitia mpango unaojulikana kama Future of Flight Series.

Teknolojia hii inalenga kupunguza foleni, kurahisisha usafiri wa mijini na kusafirisha abiria pamoja na mizigo kwa kutumia nishati ya umeme.

 Je, Tanzania inaweza kunufaika vipi?

Dar es Salaam inaweza kutumia teknolojia hii kama njia mbadala ya usafiri wa mijini.

Zanzibar inaweza kuitumia kuendeleza utalii.

Maeneo ya Serengeti, Ngorongoro na Kilimanjaro yanaweza kunufaika na huduma mpya za usafiri wa watalii.

Huduma za afya zinaweza kunufaika kupitia usafirishaji wa dawa na vifaa vya dharura.

Hata hivyo, teknolojia hii bado inahitaji majaribio, sheria za usalama, miundombinu na uwekezaji mkubwa kabla ya kuanza kutumika kwa kiwango cha kibiashara.

Tanzania inapaswa kuanza kujiandaa sasa ili isibaki kuwa mtumiaji wa teknolojia pekee, bali pia mshiriki katika mapinduzi haya ya usafiri.

 SWALI: Ungependa kuona Flying Cars zikianza kufanya kazi Dar es Salaam, Zanzibar au Dodoma?