You are currently viewing Odinga abwagwa Uenyekiti Afrika

Odinga abwagwa Uenyekiti Afrika

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameshindwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali uliofanyika leo Jumamosi, Februari 15, Raila aliondolewa katika awamu ya sita, na kushindwa katika azma yake ya kuchukua nafasi ya Mwenyekiti anayeondoka Moussa Faki.

Hili ni jaribio la pili lisilofanikiwa kwa Kenya kupata nafasi hiyo katika baraza la bara la Afrika. Mahmoud Ali Youssouf wa Djibouti aliibuka mshindi, na kuwa Mwenyekiti wa saba wa AUC tangu kuanzishwa kwa tume hiyo mwaka 2002. Mgombea wa tatu, Richard Randriamandrato wa Madagascar, alikuwa wa kwanza kuondoka katika kinyang’anyiro hicho, baada ya kushika nafasi ya mwisho.

Juhudi za kampeni za Raila zilimkosesha ushindi licha ya kampeni kali zilizongozwa na Rais William Ruto wa Kenya.

Wakati wote wa kampeni yake, Raila alizuru bara zima, akiandamana na Rais Ruto katika safari kadhaa za kidiplomasia kutafuta uungwaji mkono. Hata hivyo, wakati upigaji kura ukiendelea, uongozi wake uliteleza, na hatimaye akashindwa na Youssouf.

Leave a Reply