You are currently viewing Samia: Msitumie mabavu kuwaondoa wafanyabiashara wadogo mitaani, barabarani

Samia: Msitumie mabavu kuwaondoa wafanyabiashara wadogo mitaani, barabarani

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa mikoa kuweka utaratibu mzuri utakaowaondoa wafanyabiashara wadogo wanaofanya shughuli zao maeneo yasiyo rasmi kuhamia katika masoko makubwa.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

Amesema Serikali imefanya kazi kubwa ya kujenga masoko ya kisasa, lakini hivi sasa wafanyabiashara wadogo wamerudi kwa kasi kubwa kufanya shughuli zao mbele ya maduka na mitaani.

“Twendeni tukayasimamia haya, si kwa kuwapiga fimbo na askari mgambo au kuwanyang’anya bidhaa zao, hapana.Bali kwa mipango mizuri, ili watoke waliko, warudi katika masoko,”

“Kama ni kelele daladala hazifiki, tengenezi njia mpya ili zikashushe. Kuna mambo madogo yanayowafanya watoke na kurudi mtaani,nendeni mkasimamie na kujipanga vizuri, ‘tumerelax’, tunasubiri wakubuhu, ndio tutumie nguvu kuwaondosha,” amesisitiza Samia.