You are currently viewing TCAA yateta na wadau usafiri wa anga kuhusu maombi ya leseni

TCAA yateta na wadau usafiri wa anga kuhusu maombi ya leseni

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekutana na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kukusanya maoni kuhusu maombi ya leseni za kutoa huduma za usafiri wa anga nchini Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utoaji wa leseni hizo.

Kikao hicho cha maoni ya umma kimefanyika Novemba 11, 2026, katika ofisi za TCAA zilizopo Banana, Dar es Salaam, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, na kuhudhuriwa na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya TCAA.

Kwa mujibu wa TCAA, kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa kuimarisha uwazi, ushirikishwaji wa wadau na uzingatiaji wa taratibu katika utoaji wa leseni za huduma za usafiri wa anga.

Katika hatua nyingine, Bodi ya TCAA imeidhinisha maombi ya baadhi ya kampuni kupata leseni za kutoa huduma za usafiri wa anga na huduma za kuhudumia ndege na abiria viwanja vya ndege (Ground Handling), huku leseni hizo zikitolewa baada ya waombaji kutimiza masharti yaliyowekwa.